MoCU Repository

Hotuba ya Mhe.Prof. Peter M. Msolla (Mb), Waziri Wa Elimu Ya Juu, Sayansi na Teknolojia Katika Kumkaribisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Wakati wa Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Ushirika Na Biashara (MUCCoBS) Tarehe 18 Machi, 2006

Show simple item record

dc.contributor.author Kikuu Kishiriki Cha Ushirika Na Biashara
dc.date.accessioned 2024-11-19T17:20:10Z
dc.date.available 2024-11-19T17:20:10Z
dc.date.issued 2006
dc.identifier.uri http://repository.mocu.ac.tz/xmlui/handle/123456789/1788
dc.description.abstract Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Mawaziri, Mheshimiwa Gaudentia Kabaka, Naibu Waziri wa Elimu va Juu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Naomi Katunzi, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Mohamed Babu, Mkuu wa Mkoa, Ndugu Al Noor Kassim, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Balozi Nicholaus Kuhanga, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoinecha Kilimo, Prof. Anselm Lwoga, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Chambo, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Ndugu Waalikwa, Wanajumuiya ya Chuo, Mabibi na Mabwana. 1. Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kwa kuungana na Uongozi wa Chuo kwa kutoa pongeza za dhati kwako Mheshimiwa Rais kwa ushindi mkubwa ulioupata kaıika uchaguzi uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2005 na hatimaye kuteuliwa kuwa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Nne. TUNASEMA HONGERA. Mheshimiwa Rais, uongozi wako wa takriban miezi mtatu, tayari umekwisha, kuna na kuwagusa wananchi walio wengi hasa pale ambapo umeamua kutembelea binafsi kila Wizara kuona shughuli zao na haıimaye kutoa maagizo rami badala ya kukaa Ikulu na kusubiri laarifa kuloka kwa Watendaji. Huu ni uongozi wa kulembelea maeneo husika (Management by Walking, MBWA) ni wa kipekcc. TUNAKUPONGEZA SANA. 2. Pili , niruhus nichukue nafasi hii ya pekee kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba ya Jumuiya ya Chuo hiki kutoa shukrani za dhati kwak kwa kukubali licha ya shighuli nyingi ulizo nazo za taifa na kimatifa kuja kuzindua rasmi Chuo hii. TUNASEMA AHSANTE SANA! 3. Mheshimiwa Rais, Uzinduzi wa Chuo hiki Kikkuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) unafanya jumla ya Vyuo Vikuu vya Umma kuwa VITANO na Vyuo Vikuu vya Vishiriki vya Umma kuwa VITANO. Aidha, napenda kukufahamisha ya kwamba kuna Vyuo Vikuu binafsi KUMI na Vyuo Vikuu Vishiriki binafsi TISA, hivyo kufanya Vyuo Vikuu nchini kufika 29. Kutokana na ongezeko Ia idadi ya vyuo vikuu, kumekuwepo na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu Kutoka 17,323 mwaka 2000/01 hadi kufikia 36,870 mwaka 2004/05, ikiwa ni ongezeko Ia wanafunzi 19,547 (53%). Hivyo uzinduzi wa Chuo hiki leo unadhihirisha azma va serikali ya kupanua Elimu ya Juu kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005 yenye lengo Ia kuwawezesha asilimia 12.5% ya wanaomaliza Kidato cha Sita kupata nafasi ya kuendela na masomo katika Vyuo Vikuu, taasisi za Teknolojia na Taasisi nyingine za Elimu va Juu. 4. Mheshimiwa Rais, Wizara imezingatia maagizo yako uliyoyatoa ulipotembelea Wizara ya Elimu va Juu, Sayansi na Teknolojia tarehe 01 Februari, 2006 kwamba katika kupanua elimu ya juu, tuhakikishe kuwa vyuo vilivyokuwa vikitoa mafunzo YA kati vinaendelea kuFanya hivyo badala ya kuvigeuza vyote kuwa Vyuo Vikuu kwani wahitimu wa mafunzo ya kati bado wanahitajika kwa maendeleo ya nchi vetu. 5. Mheshimiwa rais, kutokana na maelezo hayo hapo juu, nafurahi kukufahamisha ya kwamba Chuo hiki kitaendelea na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa awali kabla va kupanda hadhi ya kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Aidha, upandaji huu wa hadhi ya Chuo hiki umekiongezea uwezo wa kutoa mafunzo hayo katika ngazi za Cheti, Stashahada ya Kawaida, Stashahada ya Uzamili, Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Udaktari wa Falsafa. Napenda kukuhakikishia ya kwamba mafunzo yote yanayotolewa kakika Chuo hiki yanalenga kuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005. 6. Mheshimiwa Rais, baada ya kusema hayo machache, kwa heshima na taadhima, sasa nakuomba nikukaribishe uweze kuzungumza na umma huu na hatimaye kutoa tamko Ia kukizindua rasmi CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA USHIRIKA NA BIASHARA. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Moshi University College of Co-operative and Business Studies en_US
dc.subject Hotuba en_US
dc.subject Elimu en_US
dc.subject Sayansi en_US
dc.subject Teknolojia en_US
dc.subject Tanzania en_US
dc.title Hotuba ya Mhe.Prof. Peter M. Msolla (Mb), Waziri Wa Elimu Ya Juu, Sayansi na Teknolojia Katika Kumkaribisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Wakati wa Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Ushirika Na Biashara (MUCCoBS) Tarehe 18 Machi, 2006 en_US
dc.type Other en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search MoCU IR


Advanced Search

Browse

My Account