Abstract:
Andiko hili limelenga kujenga uelewa wa ushirika kama falsafa, misingi na ueneaji wake
nchini Tanzania. Pia kujenga uelewa wa ushirika kwa ujumla wake ambao umekuwa
ukikumbwa na vikwazo na majanga ili kuona nii kifanyike katika kuleta ukombozi wa ukuaji
wa ushirika nhini Tanzania. Msomaji, msikilizaji na mtumiaji hana budi kujua kwamba, andiko
hili halilengi kujenga uchochezi bali kuleta uelewa. Pia yaliyomo humu ndani ni matokeo ya
uzoefu na udadisi wa mwandishi. Andiko hili lisitumiwe tofauti na mantiki na makusudio ya
kujenga uelewa na kuibua majadiliano ndani ya kongamano na kwa mtumiaji wa hapo badae.