Abstract:
Mhcshimixsa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Waziri wa Elimu ya
Juu, Sayansi na Teknolojia,
Waheshimiwa Mawaziri,
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo,
Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi
Wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Ushirika na Biashara,
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Ushirika na Biashara Moshi,
Viongozi mbalimbali wa Chuo,
Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wadau wa Elimu ya Juu,
Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wadau wa Ushirika, Wageni
Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Mheshimiwa Rais,
Kazi yangu kuu leo ni kutoa shukrani kwa kazi uliyomaliza kuifanya sasa hivi, kwani wenzangu
wengine wameishazungumza mengi kuhusu tukio hili la leo. Lakini kabla ya kutoa neno la shukrani, ninaomba kuungana na Watanzania wenzangu kukupongeza wewe binafsi na chama cha CCM kwa
kupala ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkuu uliopita. Ushindi huu umeidhihirishia dunia nzima
kwamba wewe, kwa hakika, ni Iulu iliyokuwa ikisakwa na Watanzania. Baada ya pongezi hizi,
Mheshimiwa Rais, ninaomba sasa nichukue fursa hii kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara- Moshi kutoa shukurani nyingi
kwako, kwanza kwa kukubali kuja kutuzindulia Chuo hiki kipya.
Mheshimiwa Rais, tulipokuwa tunafanya mipango ya kukualika hapa, tulisita kidogo na kuwa na
wasiwasi. Tulisita kwa sababu tulijiuliza mara nyingi kama kweli itawezekana wewe kuja hapa binafsi
katika kipindi ambacho ndio kwamba unaanza kazi yako mpya na ngumu ya kulihudutnia hili. Lakini
2
tulijipa moyo kwa kusukumwa no imani yetu kwako kwa kuwa Rais anayejali ntatukio yoyote ya kimaendeleo, kama hili tunaloshuhudia leo.
Kwa mtu mwenye kazi nyingi kama wewe, yumkini ulikuwa umeshaandaa ratiba yako ya kazi na
mambo muhimu ya kufanya. Tunajua, kwa uhakika, kwamba mwaliko wetu haukuwepo Kwenye
rativba ya kazi zako. Kwa hiyo, inaleta faraja kuona kuwa mara mwaliko ulipkufikia uliufikiria na kwa
upendo wako mkubwa ukauweka Kwenye ratiba ya kazi zako.
Mheshimiwa Rais, hii peke yake ni ushahidi wa kutosha wa jinsi unavyothamini jitihada mbalimbali
za wananchi na taasisi zao za kutaka kuimarisha huduma kwa Watanzania. Kukubali kwako kuja
kuzindua Chuo hiki ni uthibitisho kuwa unaafiki juhudi na michango ya watu na taasisi mbalimbali
katika mchakato wa kukifikisha Chuo hiki katika hadhi yake ya sasa. Kwa niaba ya wadau na wote
wanaokitakia mema Chuo hiki, ninasema "ahsante sana kwa kukubali mwaliko wetu".
Aidha, Mheshimiwa Rais, Sisi tuliobahatika kualikwa kushuhudia tukio hili kubwa, tumefarijika
kupata nafasi ya kukuona na kukusikia ukiongea kwa karibu, na hasa ukiwa ni kiongozi wa Ngazi ya
Juu kabisa hapa nchini. Ukubwa wa umati uliohudhuria hapa unadhihirisha kuwa Watanzania wengi
bado wana shauku kubwa ya kukusikiliza na kukuona kwa karibu. Ujii wako hapa ni furaha kwa watu
wengi wa Mkoa wa Kilimanjaro na majirani zao. Kwa hiyo, ungekataa mwaliko wetu, umati wote huu hapa ungebaki umefadhaika.
Pili, Mheshimiwa Rais, uzinduzi wa leo ni kumbukumbu muhimu uliyoiweka katika historia ya Elimu
ya Juu hapa nchini. Tumepata fursa ya kusikia nasaha zako, maagizo yako, matarajio yako na
changamoto mbalimbali zinazoihusu sekta ya Elimu ya Juu kwa ujumla na Sekta ya Ushirika. Kwa
jinsi baadhi ya changamoto hizo zilivyonigusa binafsi, ninaomba nirejee baadhi yake hapa.
Changamoto mojawapo ilihusu vigezo vya kuzingatia wakati taasisi mbalimbali zinapoamua
kuanzisha Vyuo vya Elimu ya Juu.
Ni kweli, Mheshimiwa Rais kama ulivyosema, kuna hatari ya kuanzisha vyuo vikuu kama fasheni.
Ukisikia, mathalan, nchi fulani wameanzisha Chuo Kikuu cha Unajimu na Sayansi za Nyota, haraka
haraka na wewe unaanzisha Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mwezi na Jua! Wahitimu wakimaliza
programu hizo za Nyota na Jua wanakuwa kama samaki aliyetolewa baharini na kuwekwa ardhini nchi
kavu! Hawawezi kusaidia watu wao katika maendcleo. Huu utakuwa ni upungufu mkubwa kwa wadau
na wahusika wengine katika kubuni mikakati ya maendeleo halisi ya Watanzania.