Abstract:
Taasisi ya ushirika ina umri wa miaka 168, tangu ilipoibuliwa huko Rochdale
Uingereza. Ushirika huu si sawa sana na ule wa jadi, ulioishi barani Afrika kwa muda mrefu
huko nyuma, ingawa baadhi ya maudhui yanakaribiana.Dhana ya ushirika wa jadi, na şuala
la watu kushirikiana halikuwa na mjadala kwa sababu lilikuwa ni tendo la kanuni za jadi
na lililenga kuihifadhi jamii ili iendelee kuishi kwa vile kushirikiana kulikuwa ni sehemu
ya maisha ya uchumi wa kujikimu ambao ulikuwa hauzalishi ziada. Ushirika huu
ulilazimika na bila kufanya hivyo, jamii ilikuwa hatarini kupotea kwa kukosa usalama wa
chakula. Watafiti kama Craig, 1976, wameuita ushirika moja kwa moja au (automatic cooperation) au ushirikajadi.