Abstract:
Ujasirishi ni dhana ambayo imeingia katika msamiati wa ushirika hivi karibuni
(Chambo 2001) hasa baada ya mjadala wa miaka thelathini ya ushirika
unaosimamiwa moja kwa moja na Serikali. Mjadala huo umekuwa ukizingatia
mambo mawili makubwa: Kwanza, ilijidhihirisha wazi wazi kuwa ushirika
'unaosimamiwa na serikali moja kwa moja utaendelea kuwa tegemezi na kwahiyo
utashindwa kuleta maendeleo ya uchumi kwa wanachama wake. Lakini upande wa
pili unaodai hoja ya ujasirishi unazungumzia hali halisi kuwa ushirika kama asasi ya
wanachama, baada ya kuondoka katika uongozi wa serikali, unahitaji wanachama
walioandaliwa katika uchumi wa kujitegemea. Ushirika unaojitegemea unahitaji
wanachama waliojasirika.